Makala Mbalimbali

Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

RAIS DK. SAMIA AZINDUA BANDARI KAVU YA KWALA NA SAFARI ZA MIZIGO ZA SGR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameandika historia mpya ya mageuzi ya kiuchumi kupitia sekta ya usafirishaji, hii ni baada ya kuzindua rasmi Bandari Kavu ya Kwala iliyopo Mkoani Pwani, pamoja na kuzindua rasmi kwa safari za mizigo kwa kutumia Reli ya Kisasa (SGR), ifikapo Agosti 4, 2025.

RAIS SAMIA AZINDUA DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameandika ukurasa mpya katika historia ya maendeleo ya taifa kwa kuzindua rasmi Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

RAIS DK. SAMIA SULUHU HASSAN ATAKA UWEKEZAJI ZAIDI NA USIMAMIZI WA KILIMO NCHINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza Wakuu wa Mikoa kote nchini kusimamia ipasavyo sekta ya kilimo kwa kuhakikisha inakuwa kipaumbele katika maeneo yao, ikiwa ni hatua ya kuimarisha uzalishaji na mchango wa kilimo katika uchumi wa taifa.

HOTUBA YA KIHISTORIA YA RAIS DK. SAMIA SULUHU HASSAN KULIHUTUBIA BUNGE LA 12 LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Katika kilele cha kufunga pazia la Bunge la 12, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan, ametoa hotuba ya kihistoria iliyochukua takribani saa mbili na nusu, akitoa mwelekeo wa taifa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu pamoja na taarifa ya utekelezaji wa ahadi na miradi ya maendeleo kwa miaka minne toka alipoingia madarakani.

MRADI WA MAJI WA SHILINGI BILIONI 12.8 WAZINDULIWA LAMADI – SIMIYU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezindua rasmi mradi mkubwa wa maji katika kata ya Lamadi, Wilaya ya Busega, mkoani Simiyu. Mradi huo umegharimu shilingi bilioni 12.8 na unalenga kuhudumia zaidi ya wananchi 85,000 kutoka vijiji vya Lamadi, Lutubiga na Mkula.

RAIS SAMIA AZINDUA DARAJA LA J.P. MAGUFULI – KIGONGO–BUSISI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezindua rasmi Daraja la J.P. Magufuli (Kigongo–Busisi) ambalo ni sehemu ya miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita.

RAIS SAMIA: ELIMU YA UFUNDI NI MLANGO WA AJIRA KWA VIJANA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali imeamua kuipa msukumo mkubwa elimu ya amali na ufundi ili kuwawezesha vijana kupata ujuzi utakaowasaidia kujiajiri au kuajiriwa moja kwa moja baada ya kuhitimu sekondari.

RAIS DKT. SAMIA ASHIRIKI SHEREHE YA KUFUNGA KOZI YA MAAFISA NA WAKAGUZI WASAIDIZI WA JESHI LA POLISI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 9 Juni 2025, ameshiriki sherehe ya kufunga kozi ya Maafisa na Wakaguzi Wasaidizi wa Jeshi la Polisi katika viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi, Kurasini, Jijini Dar es Salaam.

RAIS SAMIA ACHANGIA MILIONI 100 KUSAIDIA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU BAGAMOYO.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amelisifu Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kwa kuonesha mfano bora wa utumishi wa dini unaogusa maisha ya watu kwa vitendo.

RAIS SAMIA ASIFU MAGEUZI YA MASHIRIKA NA TAASISI ZA UMMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameeleza kuridhishwa kwake na maendeleo yanayoshuhudiwa katika mashirika na taasisi za umma, ambapo serikali imepokea gawio na michango yenye thamani ya Shilingi trilioni 1.28.

MHE RAIS DKT, SAMIA AZINDUA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025–2030

Dodoma, Tanzania – Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk. Samia Suluhu Hassan, amezindua rasmi Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha 2025 hadi 2030,

Tanzania Yazindua Rasmi Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2024

Katika hatua ya kihistoria inayolenga kuimarisha ushawishi wa Tanzania katika medani ya kimataifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezindua rasmi Sera ya Mambo ya Nje ya mwaka 2024, tarehe 19 Mei 2024 jijini Dar es salaam.

or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook