KIPAUMBELE CHETU NI AMANI, KABLA NA BAADA YA UCHAGUZI.

Scroll Down To Discover
Font size:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza umuhimu wa watanzania wote kulinda amani ya taifa hasa kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025. Akiwa mgeni rasmi katika Kongamano la Amani lililoandaliwa na Umoja wa Maimamu Tanzania (UMATA) jijini Dar es Salaam tarehe 24 Agosti 2025, Mhe, Rais ameeleza kuwa amani ndiyo urithi mkubwa wa taifa ambao unapaswa kuendelezwa na kulindwa kwa gharama yoyote.

Rais Samia katika hotuba yake ameeleza kuwa mara nyingi wakati wa uchaguzi baadhi ya watu hutumia mazingira hayo kama mwanya wa kuleta vurugu, jambo linaloweza kuhatarisha mshikamano wa taifa. Mhe rais ameeleza kuwa uchaguzi ni utaratibu wa kidemokrasia wa kuchagua viongozi, na kamwe usiwe chanzo cha migogoro au mifarakano.

Aidha, Rais amekemea tabia ya baadhi ya wanasiasa wenye tamaa ya madaraka wanaosahau maslahi ya taifa na kuangalia maslahi yao binafsi huku akitoa rai kwa viongozi na wananchi wote kuendelea kushikilia maadili, mshikamano na mshikikano wa kitaifa ili kuimarisha umoja wa Watanzania.

Viongozi wa dini pia wametoa pongezi kwa Rais Samia kwa mchango wake mkubwa katika kuimarisha maadili kupitia elimu, hususan kwa kuhakikisha masomo ya dini yanajumuishwa kwenye mtaala mpya wa elimu wakieleza kuwa hatua hiyo itawezesha vijana kupata msingi wa maadili bora na pia kutoa ajira kwa walimu wa dini nchini.

Kupitia ujumbe wake, Rais Samia amelikumbusha kuwa taifa tusipolinda amani, rasilimali nyingi hutumika katika kusuluhisha migogoro badala ya kuendesha maendeleo na kusisitiza kuwa Tanzania ni kubwa kuliko maslahi ya mtu mmoja mmoja na kwamba kila Mtanzania ana wajibu wa kushiriki katika kuilinda na kuithamini.

or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook