Rais Samia awaasa waandishi: kalamu ziendelee kulinda na kujenga taifa
MAY 2025Katika hafla ya utoaji wa Tuzo za Waandishi wa Habari (Samia Kalamu Awards) iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewahimiza waandishi wa habari kutumia kalamu zao kama nyenzo ya kuimarisha mshikamano wa kitaifa na kuchochea maendeleo, hasa tunapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu.





