Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ainua uchumi na huduma za afya wilaya ya Temeke

Scroll Down To Discover
Font size:

Katika ziara ya Dira ya Samia kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Sixtus Mapunda alitoa maelezo ya kina kuhusu juhudi za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha uchumi na huduma za afya za Wilaya ya Temeke.

Alifafanua namna ambavyo serikali chini ya uongozi wa Mhe. Rais Samia imewekeza katika kuboresha miundombinu ya barabara, elimu, afya, na michezo, hatua ambazo zimeleta maendeleo makubwa kwa wakazi wa Temeke.

Alionyesha umuhimu wa miradi kama ujenzi wa Barabara ya Kilwa na Barabara ya Mwendo Kasi, ambayo imekuwa kiungo muhimu katika kuunganisha Wilaya ya Temeke na maeneo mengine. Miradi hii ya miundombinu imechangia sana kuinua uchumi wa wilaya kwa kuvutia wawekezaji na kuongeza ajira kwa vijana.

Katika upande wa afya, Mhe. Mapunda alisisitiza jinsi ambavyo serikali imeimarisha upatikanaji wa huduma za afya, ikiwemo ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya, hospitali, na zahanati katika Wilaya ya Temeke. Uboreshaji huu wa huduma za afya umewezesha wananchi kupata matibabu bora na kwa wakati, hivyo kuboresha maisha yao kwa ujumla.

Pia, alieleza jinsi miradi hii imeifanya Wilaya ya Temeke kuwa kitovu cha biashara, ikiwezesha utoaji wa huduma kwa mikoa ya kusini kama Lindi na Mtwara. Jitihada za Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan zimeimarisha upatikanaji wa huduma bora za afya na elimu, na pia zimeleta mabadiliko makubwa katika sekta ya michezo, jambo ambalo limeongeza ari kwa vijana wa Temeke.

or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook