Rais anayejenga reli ya kisasa yenye mtandao mrefu kuliko wowote Afrika na wa tano duniani

Scroll Down To Discover
Font size:

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan Hassan, ameingia katika historia ya kuwa Rais anayejenga reli ya kisasa yenye mtandao mrefu kuliko wowote Afrika na wa tano duniani.

Wakati Serikali ya Awamu ya Sita inaingia madarakani, ujenzi wa mradi wa SGR ulikuwa ukitekelezwa katika vipande viwili vya Dar es Salaam hadi Morogoro ambapo utekelezaji wake ulikuwa umefikia 83.55% huku Morogoro hadi Makatupora ulikuwa umefika 57.57%. Vipande vyote ni jumla ya Kilomita 722 vyenye thamani ya sh. trilioni 7.4 na malipo yalikuwa dola bilioni 2.78 sawa na sh. trilioni 4.4. Kwa sasa utekelezaji wa vipande hivyo umefikia asilimia 99.03 kwa kipande cha kwanza na 96.8 kwa kipande cha pili.

Licha ya kukamilisha kazi ilivyokuwa imeanza, serikali imeanzisha ujenzi wa reli hiyo kwa vipande vipya vitano zaidi ambapo vitatu ni katika kukamilisha ujenzi wa reli ya SGR awamu ya kwanza kati ya Dar es salaam na Mwanza ambavyo ni Makutupora hadi Tabora (KM 368) ambapo ujenzi umefikia asilimia 14.39. Vipende vingine ni Tabora hadi saka (KM 165) ujenzi wake umefikia asilimia 5.86 na Isaka hadi Mwanza (KM 341) ujenzi wake umefikia asilimia 60.

Pamoja na ujenzi huo, serikali imeanza utekelezaji wa ujenzi wa reli ya SGR ya awamu ya pili kwa vipande vya Tabora hadi Kigoma (Km 506) ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 5.84 na kwa upande wa Uvinza hadi Musongati (Km 367) kuunganisha Bandari ya Dar es Salaam na soko la Burundi na DRC taratibu za ununuzi wa mkandarasi zinaendelea. Hii inafanya jumla ya kilomita 1,560 za ujenzi wa SGR kutekelezwa ndani ya Serikali ya Awamu ya Sita, sawa na asilimia 68.4 ya ujenzi unaoendelea. Thamani ya Uwekezaji huo imefikia sh. trilioni 23.3 ukiondoa kipande cha Uvinza hadi Musongati ambacho kipo katika hatua ya ununuzi. Jumla ya sh. Trilioni 10.53 zimeshalipwa kwa wakandarasl wanaotekeleza kama hati za malipo na malipo ya awali kwa vipande vipya.

Mbali ya ujenzi wa Miundornbinu, Serikali ya Awamu ya Sita imeweza kutekeleza kwa vitendo kwa kununua vitendea kazi ikiwemo vichwa 19 ya umeme, mabehewa ya abiria 89, treni za kisasa (EMU) seti 10 na mabehewa ya mizigo 1430, thamani ya uwekezaji huo ni sh. trilioni 1.3. Tayari vichwa 17, mabehewa 65, seti tatu za EMU zimewasili na majaribio ya kiufundi yanaendelea ikiwa sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa kuhakikisha kuwa miundombinu ya rell inatumika pasavyo kuchochea shughuli za kiuchumi.

#DiraYaSamia

or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook