SERIKALI YAJENGA SHULE MPYA 26 ZA SEKONDARI ZA BWENI NA SAYANSI KWA AJILI YA WANAFUNZI WA KIKE NCHINI

Scroll Down To Discover
Font size:

Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuboresha sekta ya elimu kwa kuwekeza na kufanya ujenzi na ukarabati wa miundombinu kwenye shule na vyuo, Hadi sasa serikali ipo katika hatua za mwisho kukamilisha kwa asilimia 100 mradi wa ujenzi wa Shule 26 za Wasichana za Sayansi za Mikoa zinazojengwa kupitia mradi wa Kuimarisha Elimu ya Sekondari (SEQUIP).

Mradi huu ni sehemu ya jitihada za Serikali ya Rais Samia katika kuboresha elimu kwa wanafunzi wa kike kwa ku- hakikisha upatikanaji wa mazingira bora ya kujifunzia na kuongeza fursa za kupata elimu, huku ukilenga katika Kuboresha Elimu ya Sekondari nchini na kuboresha mazin- gira ya kufundishia na kujifunzia katika shule za Sekondari na kuhakikisha usawa wa kijinsia katika upatikanaji wa elimu.

Malengo mahususi ni Pamoja na;-

- Kuongeza fursa ya upatikanaji wa Elimu ya Sekondari,

- Kuweka mazingira salama ya Elimu kwa wasichana waliopo katika Shule za Sekondari; na

- Kuhakikisha wanafunzi wote wanaoanza masomo ya se- kondari wanamaliza Elimu ya Sekondari.

Julai 17, 2024 wakati wa ziara ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan mkoani Rukwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa alisema kuwa Serikali imekwishatoa Shilingi Bilioni 104 kati ya Sh.Bilioni 106.6 zilizotengwa kwenye bajeti kwa ajili ya ujenzi wa Shule hizo za Sekondari za Wasichana sawa na asilimia 98.

Mhe. Rais Samia aliidhinisha jumla ya Shilingi Trillioni 1.2 chini ya mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya Shule za Sekondari nchini na mpaka sasa shule za Sekond- ari za Kata 402 zimeshajengwa ikiwa ni pamoja na shule hizo 26 maalum za Wasichana ambazo tayari zimeanza kupokea wanafunzi.

Mbali ya ujenzi wa shule hizo na Ili kuleta ufanisi katika utoaji wa elimu bora mradi huo umewezesha utoaji wa mafunzo kazini kwa walimu wapatao 25,109 wa masomo ya Sayansi na Hisabati nchini, Pia Wizara kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania imechapa na kusambaza vitabu vya Hisa- bati na Sayansi 2,681,800 kwa shule zote za Sekondari nchini, Ununuzi wa vifaa vya TEHAMA kwa ajili ya kuimari- sha ufundishaji na ujifunzaji kwa njia ya TEHAMA, Ununuzi wa vifaa vya Maabara kwa ajili ya kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji wa masomo ya sayansi.

or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook