Utafiti uliofanyika awali mwaka 2008 na baadae utafiti wa kina mwaka 2010-2013 ulionyesha kuwa katika kata ya Engaruka, wilaya ya Monduli Mkoani Arusha kuna uwepo wa magadi soda ya kutosha kutumika kote nchini na hata kuuzwa nje ya nchi.
Utafiti huu ulifanywa na kusimamiwa na Shirika la Taifa la Maendeleo ( NDC) kwa kushirikiana na wakala wa jiolojia Tanzania ( GST). Mradi huu ni moja ya miradi 17 ambayo imepewa kipaumbele katika Serikali ya awamu ya sita

Shirika la Taifa la Maendeleo ( NDC) ambaye ni mwekezaji kwa niaba ya Serikali ameshakamilisha vigezo vyote na kwa sasa limebaki zoezi la kulipa fidia ili mradi huo uanze kutekelezwa rasmi na hapa pongezi nyingi ziende kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tazania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kusaidia kuendeleza mradi huu kwa kutoa fedha kwa ajili ya fidia ili mradi utekelezaji uanze mara moja.

Mradi hu ambao utakuwa na uwezo wa kuzalisha tani milioni moja kwa mwaka kikiwa ni kiwango kitakachotosha kwa matumizi ya ndani ya nchi na hata nje ya nchi jambo ambalo litaitangaza Tanzania kimataifa katika biashara ya magadi soda. Mradi huu pia utakuwa na manufaa kwa wakazi wa eneo la Engaruka kwenye suala la ajira, miundombinu ya eneo hilo la uzalishaji na pia kuongezeka kwa wigo wa biashara katika eneo hilo hali itakayopelekea kukua kwa uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla
Magadi ni moja ya malighafi ambazo zina umuhimu sana katika sehemu mbalimbali kama vile katika viwanda vya vioo, viwanda vya mboleo, kutengeneza sabuni na manukato, vyakula na vinywaji, utengenezaji wa makaratasi, rangi, pamoja na utengenezaji wa dawa na hivyo kuufanya mradi huu kuwa na umuhimu sana kwa kuwa utaipunguzia Serikali gharama za kuagiza magadi soda nje ya nchi.
Changamoto kubwa hapo awali ilikuwa ni wasiwasi wa mradi huo kuwaondosha ndege wa asili wanaojulikana kama flamingo katika eneo la ziwa Natron lakini baada ya utafiti na uchunguzi wa kimazingira, mradi huo hautakuwa na adhari kwa ndege hao na wananchi wanapaswa kuondoa wasiwasi na kwa pamoja kushirikiana na Serikali katika kukamilisha mradi huu ambao utakwenda kubadilisha maisha yao.