12 AUG 2025

Ustahamilivu (Resilience)

Font size: 15px12px

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani mwaka 2021, aliweka wazi kuwa ustahamilivu ni nguzo muhimu katika kujenga taifa imara.

Ustahamilivu ni uwezo wa watu, jamii, na taifa kwa ujumla kukabiliana na misukosuko, majanga, na changamoto mbalimbali bila kupoteza muelekeo au matumaini. Katika kipindi cha uongozi wake wa miaka mitatu, Mhe.Rais Dkt. Samia ameweka jitihada kuboresha ustahamilivu wa wananchi kwa kuwekeza katika sekta muhimu kama afya, elimu, na miundombinu.

Kwa mfano, ameweka jitihada katika kujenga na kuboresha hospitali na vituo vya afya, kutoa vifaa na madawa muhimu, na kusimamia kampeni za chanjo ili kuhakikisha Watanzania wanakuwa na afya bora na uwezo wa kukabiliana na magonjwa mbalimbali ili kuwa na nguvu kazi ya Taifa yenye afya thabiti.

Pia, Mhe. Rais Dkt. Samia ameimarisha sekta ya kilimo kwa kuwasaidia wakulima wadogo kupitia mikopo, ruzuku kwenye pembejeo za kilimo, na teknolojia za kisasa. Hii imewasaidia wakulima kuongeza uzalishaji na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, hivyo kuongeza ustahamilivu wa taifa katika sekta ya chakula na lishe.

Katika eneo la elimu, Rais Samia ametoa kipaumbele katika kutoa elimu bora kwa watoto wa kike na wa kiume, kuhakikisha kuwa wote wanapata nafasi sawa ya kujifunza na kujiandaa kwa ajili ya maisha ya baadae.

Kupitia sera zake za elimu bure na kuboresha miundombinu ya shule, amesaidia kuongeza idadi ya watoto wanaohudhuria shule na kupata elimu bora.

Aidha, chini ya uongozi wa Mhe. Rais Samia, Serikali ya Awamu ya Sita imejenga shule za wasichana za bweni kwenye kila mkoa, hii itasaidia wasichana kupata elimu ya sekondari katika mazingira salama.

Kwa ujumla, ustahamilivu unahusu pia kuwa na jamii yenye mshikamano na umoja. Rais Samia ameendelea kuhimiza amani, upendo, na mshikamano miongoni mwa Watanzania, akiamini kuwa taifa lenye umoja ni rahisi kukabiliana na changamoto zozote zinazoweza kujitokeza.

or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook