RAIS DK. SAMIA AZINDUA BANDARI KAVU YA KWALA NA SAFARI ZA MIZIGO ZA SGR
Jul 2025Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameandika historia mpya ya mageuzi ya kiuchumi kupitia sekta ya usafirishaji, hii ni baada ya kuzindua rasmi Bandari Kavu ya Kwala iliyopo Mkoani Pwani, pamoja na kuzindua rasmi kwa safari za mizigo kwa kutumia Reli ya Kisasa (SGR), ifikapo Agosti 4, 2025.